Waziri wa kilimo nchini Tanzania, Japhet Hasunga ametangaza bei elekezi ya sukari kufuatia wafanyabiashara wasio waaminifu kuficha na kupadisha bei ya bidhaa hiyo.

Waziri Hasunga amesema bei za sukari zimepangwa kutokana na umbali wa mkoa husika ambapo kwa kigoma na katavi bei ya sukari kwa rejareja 3,200, huku Dar es Salaam ni 2,600 na kuonya mtu yeyote atakaye uza sukari kinyume na bei elekezi.

Mikoa ya Iringa, Njombe, Mwanza,Simiyu, Shinyanga, Geita, Singida,Tabaora na Dodoma bei ni (sh.2600), huku Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Pwani ,Tanga na Morogoro (sh.2700).

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma amesema kutokana na kupandishwa bei ya bidhaa hiyo kiholela serikali itachukua hatua kwa wafanyabiashara ambao watabainika kuuza kinyume cha utaratibu uliopangwa.

Mitihani kidato cha sita yaahirishwa, mlipuko wa Covid 19

”Miongoni mwa adhabu zitakazo tolewa ni kunyang’anywa leseni ya bishara kulipa faini au adhabu zote kwa pamaja , wafanyabisha wenye tabia ya kupandisha bei kiholela waache mara moja” amesema Waziri Hasunga

Waziri wa Viwanda na biashara, Innnocent Bashungwa amebainisha kuwa mamlaka zinazohusika na kupanga bei ya bidhaa zina wajibu mkubwa wa kusimamia bei kutopanda kiholela.

Zimbabwe yatangaza punguzo la bidhaa kukabili corona

DC Mjema afunguka wagonjwa wa Corona kutoroka Amana

Jaribio la kwanza dawa ya Corona limefeli
Video: Kauli za Magufuli, mawaziri wake utata, Serikali yatoa bei elekezi ya sukari

Comments

comments