Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) imetoa taarifa ya gharama mpya za kuunganisha umeme kama ilivyotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) kupitia Gazeti la Serikali taarifa namba 1020 iliyochapishwa Desemba 4, 2020.


Katika gharama hizo mpya kwa Vijijini ni Sh27,000 (haijalishi umbali toka unapochukulia umeme wala idadi ya nguzo)

Huku Mjini ikiwa kuanzia Sh272,000 (inategemea umbali toka unapochukulia umeme na idadi ya nguzo).

Tanesco imesema gharama hizi mpya zinaanza kutumika leo Januari 5, 2022.

Vifaa vya uviko 19 vyasambazwa mikoa 17
Young Africans yasaini dili nono Dar es salaam