Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petrol Nchini Kenya, imetangaza bei mpya ya mafuta ambapo katika mabadiliko hayo, lita moja ya mafuta ya petroli itauzwa kwa KSh. 179.30, bila ruzuku ikiwakilisha ongezeko la Ksh. 20.18.

Lita moja ya petroli jijini Nairobi, sasa itauzwa kwa TSh. 3469.94 (Ksh. 179.30) kutoka Ksh159 katika bei mpya iliyotangazwa na Mamlaka hiyo.

Aidha, bei ya dizeli imeongezeka kwa Ksh. 25 na itauzwa kwa Ksh. 165 jijini Nairobi, huku bei ya Mafuta ya taa ikiongezeka kwa Ksh. 20 na kuwa itauza Ksh. 147.94 jijini Nairobi zikiambatanisha asilimia 8 ya Kodi ya ongezeko la Thamani (VAT).

Ongezeko hilo, linamaanisha kuwa gharama ya maisha inatarajiwa kupanda wakati bei za bidhaa za viwandani zinapoanza kuongezeka, kwa sababu ya ongezeko linalofuata la gharama ya umeme.

Serikali ya Kenya, imesema imetumia takribani dola bilioni 1.2 katika mwaka uliopita kuweka bei ya mafuta chini kupitia ruzuku, huku bei ya bidhaa hiyo ikipanda katika soko la kimataifa.

Hata hivyo, Serikali mpya ya Rais Ruto imesema ruzuku imeondolewa kwasabau haijawasaidia wakenya, baada ya maoni katika mitandao ya kijamii kuhusu ongezeko hilo.

Rais Samia asikitishwa kifo cha Mkurugenzi Igunga
Haji Manara arudisha kombora Kamati ya Rufaa