Mkali wa nyimbo za Burger Self na Masogange, Belle 9 ambaye kwa muda mrefu amepotea kwenye game, sasa amekuja na wimbo wake mpya ambao umeleta gumzo kwa mashabiki kwa kile kinachodaiwa kuwa kaiga baadhi ya vipande na mdundo kwenye nyimbo ya msanii mkubwa Diamond Platinumz katika wimbo wake wa Salome.

Ngoma yake mpya inayofanya vizuri sasa ya ‘Give it to me’, vipande kwenye nyimbo hiyo vinafanana na mdundo alioutumia Diamond katika wimbo wake wa Salome, kitu ambacho kiliwafanya mashabiki wa msanii huyu mkongwe wa bongo fleva kumponda, japokuwa Belle 9 alikanusha uvumi huo.

Amesema ngoma yake mpya ya ‘Give it to me’ hajamuiga Diamond na Darassa kama wengi wanavyosema. Amedai kuwa kilichotokea ni yeye kuchelewa kuiachia ila utunzi na rekodi ya nyimbo hiyo ulishafanyika siku nyingi zilizopita.

”Diamond ni mdogo wangu siwezi kumuiga kwa chochote na mimi nilishaurekodi kitambo na hata ukisikiliza mashairi yangu na Salome hayaendani kwa wafuatiliaji wazuri wa muziki watakubaliana na  mimi kuwa sijawahi kuiga msanii yoyote tangu natoka, alisema,” belle 9.

Wolper na Harmonize wadaiwa kutafuta kiki
Zitto ageukia taarifa za ‘njaa’, atoa neno kwa Serikali