Mwimbaji kutoka Morogoro, Belle 9 yuko katika maandalizi ya kuwapa mashabiki wake zawadi ya mwaka mzima kwa kumfanya yeye kuuona mwaka huu kama mwaka wake.

Belle 9 ambaye hivi karibuni ameachia Remix ya wimbo wake wa Burger, ‘Movie and Selfie’ aliowashirikisha Jux, Izzo Bizness, G-Nako na Maua Sama, amesema kuwa mwaka huu amepanga kuachia album yake mpya kwa ajili ya mashabiki wake, aliyoipa jina la ‘The Year of Belle 9’.

“Mwaka huu nitaachia albam yangu mpya, inaitwa ‘The Year of Belle 9’ yaani mwaka wa Belle 9,” aliiambia Hatua Tatu ya 100.5 Times Fm jana. Hii itakua albam inayoifuatia ile ya awali ya ‘Vitamin Music’.

Katika hatua nyingine, Belle 9 ambaye hivi sasa yuko chini ya wasimamizi wapya wa muziki wake (new management), amesema kuwa endapo mkataba wake na wasimamizi hao utakafikia kikomo, yuko tayari kujiunga na label ya WCB ya Diamond Platinumz endapo watamhitaji kwa sababu anaiamini na kwamba yeye ni mfanyabiashara.

Wasiovaa Helmet kwenye Bodaboda kushtakiwa kwa 'kutaka kujiua'
Mbatia alina na adhabu za Bunge kwa wapinzani, amtupia lawama Dk. Tulia