Mfululizo wa ndoa za wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini katika miezi ya hivi karibuni umemuibua mkali wa RnB, Ben Pol ambaye ameamua kuweka wazi atakavyoishangaza dunia utakapofika wakati wake wa kuoa.

Mwimbaji huyo ambaye amewahi kulalama kwenye wimbo wake ‘Number 1 Fan’ kuwa shabiki wake wa moyo anataka kugeuka kuwa ‘baby-baby’, hali iliyosababisha aachwe na mpenzi wake, amesema kuwa siku atakapojisikia yuko tayari atamuoa mwanamke yeyote aliye mbele yake bila kuzingatia historia ya uhusiano wao!

“Mimi naamini itafika siku moja nitasema ‘sasa naoa’. Nilikuwa nawaambia washkaji zangu wanashangaa… mimi ikifika hiyo siku mimi nitamuoa mtu aliye mbele yangu muda huo. Sitakuwa na mambo yale ‘sasa tumetoka wapi, mara miaka mitatu tulikuwa pamoja,” alifunguka.

Ben ameiambia The Playlist ya 100.5 Times Fm wiki hii kuwa amegundua historia ya kuwa pamoja kwa muda mrefu kwenye mahusiano sio kigezo cha maana cha kuwafanya watu wawe kwenye ndoa itakayokuwa ya mafanikio.

“Mimi naona wakati mwingine watu wanaweza kuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu wanafahamiana, wana watoto hata wawili au watatu lakini ikifikia muda wakaja wakasalitiana… wakaachana,” alisema. “Sasa nini maana ya kujua historia yake wakati baadaye inakuja kuwa hivi… na kuna wengine wanakutana muda mchache lakini wanakuwa real (halisi) na hakuna usaliti,” aliongeza.

Hivi karibuni, Ben ameachia wimbo wake mpya alioubatiza jina la ‘Zai’ akiwa na mwimbaji kutoka Nigeria, Kiss Daniel.

Usikilize hapa:

Kim Kardashian aonja ‘joto ya jiwe’ kwa kuweka tangazo la msosi
Trump amgeuka mshauri wake kuhusu kuifanya Korea Kaskazini kama Libya

Comments

comments