Mkali wa RnB, Ben Pol jana alimvalisha pete ya uchumba mrembo kutoka Kenya, Anerlisa ambapo alitumia nafasi hiyo kuuliza swali maarufu la ‘Je, unakubali nikuoe?’ na Mkenya huyo amethibitisha kuwa alijibu ‘Ndiyo’.

Wawili hao wamefikia hatua hiyo ikiwa ni miezi michache tuangu waanzishe uhusiano wao, huku maisha yao ya kifahari yakipata umaarufu mitandaoni.

 

View this post on Instagram

 

Well… This Just Happened!!! #SheSaidYes💍

A post shared by BEN POL #PIZZΞУ (@iambenpol) on

Hata hivyo, hatua ya Ben Pol imewaamsha baadhi ya mashabiki ambao wamempongeza kwa kuchukua hatua kwa vitendo, huku wakimgeukia Diamond Platinumz ambaye amekuwa akiahidi kuwa atamuoa mrembo wa Kenya, Tanasha lakini bado hajamvisha pete.

Mashabiki hao wamekumbushia ahadi kama hizo alizokuwa akizitoa Diamond kwa Zari ambaye alimzalia watoto wawili, lakini hawakuwahi kufikia hatua ya kufunga ndoa.

Ben Pol anaonesha kufuata nyayo za Ali Kiba ambaye alifunga ndoa na Mkenya. Hivyo, kama atakamilisha hatua hiyo na Diamond pia akafanyia kazi kwa vitendo ahadi yake kwa Tanasha, Wasanii wakubwa watatu Tanzania watakuwa wameoa warembo kutoka Kenya.

Muziki wa Tanzania umevuka mipaka na sasa unakubalika zaidi nchini Kenya kulinganisha na nyakati za zamani ambapo muziki wa Kenya ndio uliokuwa ukiitikisa zaidi Bongo. Hivi sasa, sanaa imeonesha kuwaunganisha Wakenya kimuziki na hata kifamilia.

Hongera ziende kwa Ben Pol, tunawaombea Diamond na Tanasha wafanye jambo pia.

LIVE: Ziara ya Rais Magufuli mkoani Mbeya | Akihutubia Taifa
Wabunge Uganda wajiongezea mshahara

Comments

comments