Urafiki kati ya Baraka Da Prince na Ben Pol hauko kwenye wakati mzuri, hasa baada ya mkali huyo wa ‘Nisamehe’ kumchana wazi mwenzake kuhusu sakata la kupozi akiwa mtupu.

Baraka alikosoa uamuzi wa Ben Pol kuweka picha hizo kwenye mitandao ya kijamii akidai kuwa nguvu iliyotumika kuunadi mradi wa wimbo huo hazilingani hata kidogo na mradi halisi.

Akiongea na ENews ya East Africa TV, Ben alisema kuwa tayari ameshamsamehe Barakah kama mdogo wake na kwamba ataendelea kumsamehe hata kabla hajamkosea kwani mambo hayako sawa kati yao.

“Barakah mimi nilishasema nimemsamehe hata kabla hajanikosea, kwa sababu naona kuna vitu haviko sawa. Kwahiyo mimi sijishughulishi, nategemea chochote kile,” alisema Ben Pol.

Hata hivyo, Ben alieleza kuwa bado Barakah atabaki kuwa mshikaji wake ingawa hata akikutana nae wakati mwingine hugeukia upande mwingine ili asimuone. Alidai kuwa hata anapokuwa ‘amekaushiwa’ na Barakah huamua kumfuata na kumsalimia akimwambia kuwa amemuona.

Wakali hao wamekutana mara ya mwisho kwenye ngoma ya DJ D Ommy wa Clouds Fm iliopewa jina la ‘DJ’, ambao ndani yake pia yuko mkali wa RnB, Jux.

Kesi ya 'Scorpion' mtoboa macho yazidi kupigwa kalenda
Harmorapa azungumzia sakata la kuvaa gauni la Bosi wake