Baada ya kuipandisha timu ndani ya Ligi Kuu Bara na kuiongoza Gwambina kwenye jumla ya mechi 17 ikiwa nafasi ya 14 na pointi zao 19 benchi la ufundi limefutwa kazi mazima.

Kwa sasa mabosi wa Gwambina wameingia sokoni kusaka mbadala wa makocha hao, ambao wataendeleza gurudumu ndani ya kikosi hicho kinachotumia Uwanja wa Gwambina Complex.

Kocha Mkuu, Fulgence Novatus na msaidizi wake Athuman Bilal sasa wapo huru kujiunga na timu yoyote baada ya ajira zao kusitishwa rasmi Januari 4.

Mchezo wa mwisho kukaa benchi ilikuwa ni dhidi ya Biashara United ambapo ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Kwa sasa timu ipo mikononi mwa kocha Khassain Salum na Seleman Kisedi pamoja na viongozi wengine.

Mkurugenzi wa benchi la ufundi ndani ya Gwambina  FC ni Mwinyi Zahera ambaye aliwahi kuinoa Yanga.

Shule binafsi zaonywa kupandisha ada
Hakuna kuingia wala kutoka Kigali