Majuma mawili kabla ya Simba kukutana na Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara , kuna habari ambayo sasa ni gumzo mjini.

Habari kutoka ndani ya Klabu ya Simba zinaeleza kuwa Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Jackson Mayanja ameamua kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na sababu binafsi.

Taarifa zilizopatikana zinadai kuwa, Mayanja ameamua kuchukua maamuzi hayo kutokana na sababu binafsi huku ikidaiwa matatizo ya kifamilia yamechangia kuondoka kwake.

Baada ya kuwepo kwa uvumi huo Dar24 tulimtafuta Mayanja na kumuuliza, ili kupata ukweli wa jambo hilo, na jibu lake lilituthibitishia ni kweli ameondoka Simba.

“Matatizo ya kifamilia yamekua chanzo cha mimi kuachana na Simba, Nimeshakutana na viongozi na tumefikia makubaliano mazuri, naamini ninaondoka nikiwa na mahusiano mazuri na viongozi wangu,”

“Nilitamani kuendelea kufanya kazi ndani ya klabu ya Simba lakini naona muda ambao nitakua ninashughulikia masuala ya kifamilia utakua mrefu mno, hivyo nimeona ni bora nikaachia nafasi yangu Simba ili nijipe nafasi ya kumalizana na tatizo linalonikabili kwa sasa.”

“Ninawashukuru wote walionipa ushirikiano tangu nilipofika Simba, na ninaamini msimu huu mashabiki na wanachama watafurahia ubingwa, maana timu yao ipo vizuri na ina malengo ya kufanya hivyo.” Alisema Mayanja

Mayanja aliwahi kukiongoza kikosi cha Simba kama kocha mkuu msimu wa 2015/16, kabla ya kuajiriwa kwa Omog msimu uliopita.

 

Aliou Cisse apingana na ripoti ya Liverpool, amuita Mane
Bodi ya mikopo yatoa orodha ya watakaonufaika