Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imetakiwa kuwekeza katika mkoa wa Manyara ili kuwawezesha wakulima kupatia mikopo na mahitaji mengiune wananchi kwa ajili ya tija

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera alipotembelewa na ugeni huo ofisini kwake, amesema kuwa mkoa wa Manyara una fursa nyingi za uwekezaji hasa katika sekta ya Kilimo na mifugo.

“Mkoa wa Manyara una fursa nyingi sana ambazo Benki inaweza kutoa mikopo ambayo nina uhakika itarudishwa kwa wakati kwa sababu watu wa Manyara ni waaminifu sana,” amesema Bendera.

Kwa upande Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Francis Assenga amesema Serikali imeamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika  kilimo nchini.

 

Kaseja autaka utangazaji wa Radio/Tv
Video: Itazame 'Zezeta' ya Rayvanny aliyoshiriki Sugu