Rais wa Marekani Donald Trump ametoa amri ya bendera ya nchi hiyo kushushwa nusu mlingoti kwa siku tatu mfululizo, kuomboleza vifo vya Wamarekani waliokufa kutokana na virusi vya corona.

Trump ameamrisha hatua hiyo, baada ya idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa COVID-19 kukaribia 100,000 nchini humo.

Aidha Trump amesema bendera zitabakia nusu mlingoti Jumatatu ijayo ambayo ni Siku ya Mashujaa nchini humo, kuwakumbuka wale ambao wamepoteza maisha wakilitumikia jeshi la Marekani.

Imeelezwa kuwa Ingawa idadi ya vifo vya kila siku nchini humo haijaongezeka, watu bado wanaendelea kupoteza maisha, na hesabu kamili inapindukia vifo 94,500 ikitajwa kuwa ni taifa lenye vifo vingi ulimwenguni.

Wiki hii Marekani imerikodi vifo 1,300 kwa siku, vinavyotokana na virusi vya corona.

Waziri Kairuki avutiwa na uwekezaji kiwanda cha mafuta ya alizeti
Mitihani ya Kidato cha sita kuanza rasmi juni 29