Rafael Benitez amesema ilikuwa ‘heshima kubwa’ kuwa mkufunzi mkuu wa Real Madrid, siku moja baada yake kufutwa kazi klabu hiyo ya La Liga.

“Kama Mwanamadrid kutoka Madrid, anayeelewa utamaduni na maadili ya klabu hii, imekuwa heshima kubwa kufanyia kazi rangi hizi za klabu hii,” amesema kupitia taaifa.

Ameongeza: “Ningependa kushukuru kila mmoja ambaye tangu siku ya kwanza aliniunga mkono na kufanya kazi yangu kuwa rahisi.’

Mhispania Benitez, mwenye umri wa miaka 55, aliachishwa majukumu yake baada ya mkutano wa bodi ya klabu hiyo siku ya Jumatatu.

Nafasi yake ilipewa mkufunzi mkuu wa timu B, mchezaji wa zamani wa Ufaransa Zinedine Zidane.

Benitez alipoteza mechi tatu kati ya michezo 25 na kuwaongoza Real kufika hatua ya 16 katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

“Baada ya kusema hayo yote, ningependa kumtakia kila la kheri Zinedine Zidane, mrithi wangu, na wasaidizi wake. Kwa wachezaji, wakufunzi na wafanyakazi, nawatakia kila la kheri.”

Watumishi wengine Tisa watumbuliwa
FDL STARTIMES RAUNDI YA 10 WIKIENDI HII