Licha ya kupoteza mchezo wa mzunguuko wa tatu wa ligi kuu ya England kwa kufungwa mabao mawili kwa moja na Chelsea, meneja wa Newcastle Utd, Rafael Benitez ameendelea kuwa na matumaini ya kufanya vyema msimu huu na kuwataka mashabiki kuiamini timu yao.

Benitez amesema hatua ya kupoteza mchezo wa jana jumapili ni sehemu ya kuendelea kujifunza kutokana na makosa yaliyofanywa na wachezaji wake, hivyo anaamini hali hiyo haitojiridia tena katika michezo inayofuata.

Amesema ligi bado ina muendelezo mrefu, na kila timu inapaswa kupambana ikiwepo Newcastle Utd, na litakua jambo na kipuuzi kwa mashabiki wa klabu hiyo kukata tamaa, baada ya kushuka dimbani mara tatu na kuambulia alama moja pekee.

“Sioni sababu ya kukata tamaa kwa kila anaeishabikia klabu hii, ninaamini tutafanya vizuri, kwa sasa tunaendelea kujifunza kutokana na makosa tutayoyafanya na kupelekea timu pinzani kutufunga,” alisema meneja huyo kutoka Hispania.

“Lengo kubwa ni kuhakikisha timu inafanya vizuri, lakini katika mlolongo wa kufanya vizuri, wakati mwingine lazima upoteze ili kujua udhaifu ulionao, kwa sasa bado ni mapema mno kwetu kukata tamaa, matokeo mazuri yatapatikana katika michezo ijayo,” aliongeza.

Newcastle Utd imeshapoteza michezo miwili kwa kufungwa na Tottenham Hospurs na Chelsea huku akitoka sare ya bila kufungana na Cardiff city.

Bobi Wine na wenzake waachiwa huru kwa dhamana
Lugola amsweka ndani mkuu wa kituo cha Polisi