Benki Kuu ya Tanzania imechukua usimamizi wa Benki ya Twiga na kuisimamisha Bodi yake baada ya kubaini kuwa ina upungufu mkubwa wa mtaji.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, Benki Kuu imeeleza kuwa imechukua hatua hiyo kwa mujibu wa sheria ya Mabenki na Taasisi ya Mwaka 2006 kwakuwa upungufu huo wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya kifedha na amana za wateja wake.

“Kutokana na uamuzi huo, Benki Kuu ya Tanzania wameisimamisha Bodi ya Wakurugenzi na uongozi wa Benki ya Twiga na imemteua meneja msimamizi ambaye atakuwa na jukumu la kusimamia shughuli za Benki ya Twiga kwa kipindi ambacho itakuwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu,” imeeleza taarifa hiyo.

Aidha, imewaeleza kuwa kwa kipindi cha wiki moja kuanzia leo, shughuli zote za kibenki katika Benki ya Twiga zitasitishwa ili kutoa nafasi ya kupanga taratibu za uendeshaji wa benki hiyo.

Ole Sendeka amvaa Lowassa kwa kauli zake kuhusu hali ya maisha
Kikwete avunja ukimya, ataka aachwe apumzike, "nimechoka"