Benki na Taasisi za Fedha zimetakiwa kuwafikia watanzania wengi ambao wanajihusisha na shughuli za uzalishaji mali kama vile kilimo na Ufugaji, kwa kusogeza huduma zao katika maeneo ya vijijini.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Peter Mavunde wakati wa uzinduzi wa benki ya Yetu Microfinance Bank PLC katika kata ya Mngeta, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro.

Mavunde amezitaka Taasisi hizo za fedha zisaidie katika utoaji wa mikopo nafuu kwa wakulima ikiwemo mikopo ya fedha taslimu, mikopo ya zana za kilimo na mashine za uchakataji wa mazao kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali kupitia uchumi wa Viwanda.

Pia emewataka wananchi wa kata ya Mngeta kuitumia fursa hiyo kuboresha kilimo chao kwa kulima kwa njia za kisasa na pia kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya uchakataji mazao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki, Millinga amemuelezea Naibu waziri kwamba wameshaanza mchakato wa kuwakopesha wakulima mashine za uchakataji wa mazao na watatanua wigo zaidi ili kuwafikia wakulima wengi zaidi.

Sigara yasababisha watu 123 kuteketea kwa moto
Lori lalipuka na kuteketeza watu 123, Pakistan