Taasisi ya kifedha ya Benki ya CRDB imetangaza kuanza kutoa huduma ya kibenki inayoendana na matakwa ya imani ya dini ya Kiislamu katika matawi yake yote hapa nchini ili kuhakikisha wateja wake wanaoamini katika imaani hiyo wanapata fursa ya kuitumia bila manung’uniko katika nafsi zao.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa fedha na wa benki hiyo, Frederick Nshekanabo katika Iftari iliyoandaliwa na benki hiyo tawi la Bukoba kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Jafary kwaajili ya wateja wake ambapo amesema kuwa benki ya CRDB imedhamilia kuanzisha huduma ya ISLAMIC BANKING ili kuweza kuwapa fursa zaidi Waislamu kuitumia benki hiyo.

Amesema kuwa benki inatambua mchango mkubwa wa wateja wake hasa Waislamu katika matawi yake yote hivyo wanayo sababu ya kujitahidi na kuhakikisha wanayatimiza matakwa ya wateja wao ili kuweza kuendana na kauli mbiu yao ya CRDB BANK, BANK INAYOMSIKILIZA MTEJA. CRDB BANK ULIPO TUPO.

“Tunamshukuru mungu kwa kuweza kujumuika pamoja katika Iftari hii, nipende kusema kuwashukuru kwa kuendelea kuichagua benki ya CRDB kuwa chaguo lenu namba moja. Niendelee kuwahakikishia kuwa tutaendelea kuwasikiliza na kuwahudumia ili kurahisisha upatikanaji wa huduma iliyo bora.” Amesema Nshekenabo.

Kwa upande wake sheikhe wa mkoa Kagera, Alhajj Kharuna Kichwabuta ameishukuru benki hiyo kwa kuwakutanisha pamoja wateja wake namna inavyoendelea kuwahudumia kwa kuzingatia misingi ya haki na maadili yaliyobora ambapo amesema kuwa akaunti zote za Baraza kuu la Waislamu Bakwata zipo katika benki hiyo.

Naye Professa Faustin Kamuzola katibu tawala wa mkoa Kagera aliye muwakirisha mkuu wa mkoa huo Brigedia Jenerali Marco Gaguti aliwasihi wananchi wa mkoa huo kuitumia benki ya CRDB katika masuala ya Kifedha kwa kuwa wanatoa elimu na ushauri wa namna gani unaweza kuitumia fedha kwenye miradi mbalimbali ili kuepuka hasara.

Benki ya CRDB imesema itaendelea kuboresha huduma zake zote ikiwemo kuongeza matawi na kuwataka wateja wake kuendelea kuzitumia huduma janja za simu banking na tembo card kwa kuwa zinarahisisha Muda katika matumizi.

Kila kijiji kitakachopitiwa na bomba la mafuta kupatiwa umeme- Mgalu
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 5, 2019

Comments

comments