BENKI ya Taifa ya Biashara Tanzania (NBC) imetoa Sh. 50 Milioni kwa ajili ya kuisaidia ujenzi wa kiwanja cha kisasa kitakacho jengwa eneo la Mtipa nje kidogo ya Manispaa ya Singida.

Kiwanja hicho kitakuwa kikimilikiwa na Timu ya Singida Big Star ambayo imeingia msimu huu kushiriki mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kupanda daraja.

Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea fedha hizo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge ameishukuru benki hiyo kwa kusikia kilio cha muda mrefu cha wadau wa michezo mkoani hapa na kukubali kuchangia kiasi hicho cha fedha.

“Maombi ya wadau wa mkoa, chama na wawakilishi wetu Bbenki ya NBC wameyasikia na kuamua kutupatia kiasi hiki cha fedha hongereni sana NBC tutahakikisha fedha hizi zinakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa na si vinginevyo” alisema Mahenge.

Mahenge alisema anatamani sana kuona sasa kuna kuwa na mechi za mfululizo zikifanyika katika uwanja wa zamani na huo mpya ukikamilika ili wananchi wa Mkoa wa Singida wafaidike kwa kupata burudani ya mechi mbalimbali.

Habari kuu katika magazeti ya leo Juni 11, 2022
Italia kuanzisha upya safari za ndege Zanzibar