Benki ya Tanzania Postal Bank (TPB) imeandaa mkutano wa mabenki ya Akiba ya AfrIka Mashariki ili kuweza kujadili changamoto mbalimbali.

Katika mkutano huo uliofanyika visiwani Zanzibar na kuhudhuliwa na wajumbe wa benki za Akiba kutoka katika nchi za Uganda na Kenya ulikuwa na lengo la kujadili changamoto na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika nchi za Afrika Mashariki.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugezi wa Benki ya TPB Dkt. Edmund Mndolwa amewasisitiza wajumbe kutoka katika nchi hizo kuchangamkia fursa za uwekezaji katika nyanja mbalimbali.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi, akichangia hoja katika mkutano mkuu wa benki za akiba Afrika Mashariki, amesema kuwa endapo kama wajumbe hao watazifanyia kazi fursa katika maeneo ya uwekezaji basi benki hizo zitaweza kutanua wigo na kuwa mkubwa zaidi.

Serikali yatoa milioni 500 ujenzi wa hospitali Wanging'ombe
Majaliwa afungua kiwanja kipya cha Baseball jijini Dar