Benki Kuu nchini Uganda imepiga marufuku tabia iliyoibuka ya baadhi ya wafuasi wa mwanasiasa machahari, Bobi Wine kuandika jumbe kwenye noti za fedha kwani ni uhalifu na vianaashiria ukosefu wa maadili.

Baadhi ya raia wa Uganda wamekuwa wakiandika jumbe za kisiasa kwenye noti za fedha, ambapo jumbe nyingi ni za kushawishi kuchaguliwa kwa Mbunge Bobi Wine kuwa Rais katika uchaguzi wa 2021.

Aidha benki hiyo imefafanua kwamba kwa kuandika maneno kwenye fedha, kunashusha thamani yake, na kuharibu ubora na ulinzi wake taarifa iliyotolewa na banki hiyo imeeleza “. Benki imebaini kuhusu wasiwasi kwa habari kadhaa zianazovuma kwenye mitandao ya kijamii zinazozunguka picha za sarafu za Uganda zikiwa na ujumbe wa kampeni za kisiasa. Kwa kweli hii inaweka hali ya wasi wasi kwa maneno ambayo yameandikwa au kuchafuliwa kwa njia yoyote”

Na kusisitiza kuwa wananchi wote wawe makini, kuandika alama kwenye noti au sarafu huingiliana na huduma za usalama.

Robert Kyagulanyi Ssentamu (Bobi wine) alichaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo baada ya kusimama kama mgombea huru mwaka juzi wilayani Kyadondo mashariki, Uganda ya kati.

Mnamo mwezi Julai 2019, Bobi Wine alitangaza nia yake ya kuwania urais nchini humo 2021, na alizindua kikosi cha kuendesha kampeni yake ya kuwania Urais.

Video: Magufuli aonya CCM kuanguka, kanisa lenye masharti ya ajabu nchini
Video: Magufuli atangaza Ndege iliyokamatwa Canada yaachiwa