Mwanahabari kutoka kituo cha Televisheni cha Citizen na aliyekuwa jaji mkuu katika shindano la East Africa Got Talent, Jeff Mwaura Koinange  ameingia katika mgogoro mkubwa na benki baada ya kukiuka sheria ya kulipa deni la zaidi ya KSh130 milioni mwaka 2019, huku benki hiyo ikiwa inataka kurejesha angalau KSh65 milioni kutoka kwenye nyumba zake.

Hali iliyopelekea kampuni ya kupiga mnada, Garam Investments  kutangaza kuzipiga mnada nyumba zake ambazo zimejengwa katika hekari 0.67 katika eneo la Kitisuru.

Mnamo Jumatatu, Aprili 6, kampuni ya kupiga mnada ilichapisha tangazo hilo katika gazeti moja nchini humo ikiwataka wale ambao wanataka mali hiyo kutuma maombi.

Katika taarifa, kampuni hiyo ya kupiga mnada iliwaomba wanaotaka kununua nyumba hizo kutoa KSh5 milioni pesa taslimu ama kupitia hundi kabla ya kuruhusiwa kutoa bei yao.

“Kipande kizima kinachotambuliwa kama L. R. NO. 7741/263 (I. R. NO. 115833) katika barabara ya Kitisuru, Kaunti ya Nairobi kimesajiliwa kwa jina Jeff Mwaura Koinange,” “Wenye hamu wanatakiwa kutoa Ksh5 milioni kupitia pesa taslimu ama hundi kabla ya kuruhusiwa kutoa beo yao,” ilisoma tangazo hilo la kampuni ya Garam Investments.

Kampuni hiyo ya kupiga mnada haijafichua thamani ya mali hiyo huku ikishikilia kwamba itanyakuliwa mnamo Aprili 28, mwaka huu.

Aidha, Mwanahabari huyo pia hajatoa sababu za mali yake kutaka kupigwa mnada na kampuni hiyo.

Lema: Serikali itoe nyumba bure wanaohudumia wagonjwa Covid 19
Rais Trump aitupia lawama WHO