Mtendaji mkuu wa klabu bingwa nchini Italia Juventus FC, Beppe Marotta amepanga kukutana na wakala wa kiungo kutoka nchini Ufaransa Paul Pogba (Mino Raiola) kwa lengo la kuzungumzia hatma ya mchezaji huyo.

Pogba amekua katika tetesi za muda mrefu za kutaka kuondoka Juventus Stadium katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi, na klabu ya Man Utd imeonyesha kuwa mstari wa mbele kutaka kumsajili kwa ada ambayo huenda ikavunja rekodi ya dunia.

Tayari Man utd wameshatuma ofa ya Euro milioni 110, lakini ilikataliwa na viongozi wa Juventus kwa madai haikuwa sawa na thamani ya kiungo huyo, ambaye alikua sehemu ya kikosi cha Ufaransa ambacho kilishindwa kutwaa ubingwa wa Euro 2016 katika ardhi ya nyumbani, mwanzoni mwa mwezi huu.

Mino Raiola

Hata hivyo imeanza kuhisiwa huenda Marotta amepanga kukutana na wakala wa mchezaji huyo, kwa ajili ya kumtaka alimalize suala la uhamisho wa Pogba kufuatia kuonekana kuwa kikwazo kwa kutaka athibitishiwe mgao wa malipo yake kama msimamzi.

Raiola anatajwa kuwa kikwazo kwa dili la usajili wa Pogba kukamilishwa mpaka sasa, kutokana na madai yake ya kutaka mgao wake wa Pauni milion 25 kutengwa pembeni na ndipo mambo mengine yafuatie.

Tajiri Wa Inter Milan Amalizana Na Roberto Mancini
Video: Makonda Atoa Ujumbe Muhimu Kwa Wakazi Wa Dar