Uongozi wa klabu ya West Bromwich Albion, imekataa dau la pauni milioni 15 kutoka kaskazini mwa jijini London, ambalo lilitumwa na klabu ya Tottenham Hotspurs, kwa lengo la kumsajili mshambuliaji Saido Berahino.

Berahino mwenye miaka 22, amekua katika mawindo ya kocha wa Spurs Mauricio Pochettino, kwa lengo la kutaka kuimrisha safu yake ya ushambuliaji msimu huu, na mara kadhaa amekuwa akionyesha matumaini ya kumpata katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Mwenyekiti wa klabu ya West Brom, Jeremy Peace amemwambia mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy hawako tayari kumuachia mshambuliaji huyo mwenye asili ya nchini Burundi kwa dau la pauni milioni 15.

Hata hivyo Peace amesisitiza kuwa katika hali ya kutaka kufanya biashara na Spurs kupitia kwa Berahino, endapo dau la paund million 25 litawasilishwa mezani kwake.

Berahino alimaliza msimu uliopita, akiwa katika orodha ya wachezaji watatu wa mwanzo kutoka nchini England waliopachika mabao mengi kwenye ligi ya nchini England ambayo iliongozwa na  Harry Kane kisha Charlie Austin.

Purukushani Za Usajili Barani Ulaya
Pique Afungiwa Michezo Minne