Mshambuliaji Dimitar Berbatov ametambulishwa rasmi kwa mashabiki wa klabu ya PAOK Salonika ya nchini Ugiriki baada ya uhamisho wake kukamilika mwanzoni mwa juma hili.

Mashabiki 10,000 waliokua wamefika kwenye uwanja wa Toumba unaomilikiwa na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya nchini Ugiriki walionyesha furaha yao kwa kupiga kelele huku wakisema karibu Berbatov.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34, amesajiliwa na klabu ya PAOK Salonika akitokea nchini Ufaransa alipokua akiitumikia klabu ya AS Monaco ambayo ilimsajili mwaka 2014 akitokea Fulham ya nchini England.

Berbatov aliyekabidhiwa jezi namba kumi ya klabu hiyo alirejesha fadhila kwa mashabiki kwa kuaambia amefurahishwa kuwa nao na ana Imani atashirikiana na wengine kufanya linalowezekana ili kufikia lengo mwishoni mwa msimu huu.

Kabla ya kukamilisha mpango wa kuelekea nchini Ugiriki Berbatov, alikua anahusishwa na mpango wa kutaka kurejea nchini England kujiunga na klabu ya Aston Villa, lakini dau la Euro million 1.6 ambazo ni sawa na paund million 1.2 lililotangazwa na PAOK Salonika liliharibu mpango huo.

Askofu Kilaini Amshangaa Dk Slaa, Sumaye Naye Anena
Wavuta Sigara Wamsaka Mshindi Messi Vs Ronaldo