Rais wa klabu ya AC Milan Silvio Berlusconi amethibitisha kuiuza klabu hiyo kwa wafanyabiashara kutoka nchini China.

Berlusconi amethibitisha kufanyika kwa biashara hiyo alipozungumza na kituo cha televisheni cha Rai 3.

Mfanyabiashara huyo maarufu nchini Italia ambaye pia aliwahi kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo, amesema kwa sasa kilichosalia ni makabidhiano ya nyaraka muhimu.

“AC Milan tayari imeshauzwa,” Alisema Berlusconi.

“Haikua kazi rahisi kwangu na kwa wanunuzi wa klabu hii, tumefanya mazungumzo ya kina ambayo yalichukua muda mrefu, na kwa bahati nzuri tumefikia hatua kubwa na ya kupendeza.

“Kwa sasa taratibu za awali zimeshakamilika na mambo mengine yanaendelea kufanywa, lakini itakapofika Disemba 13 kila kitu kitakua kimeshakamilishwa na ninaamini uongozi mpya utaanza kufanya kazi chini ya utawala wa wamiliki kutoka China. Alisisitiza Berlusconi

Virgil van Dijk Kuziba Pengo La John Stones
Dk. Bana adai uamuzi wa Ndalichako kuhusu Diploma ni dhambi ya ubaguzi