Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison, amefungiwa kucheza michezo mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kutozwa faini ya Shilingi Milion moja, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya utovu wa nidhamu ndani ya Uwanja.

Morrison ametiwa hatiani na Kamati ya saa 72, kufuatia kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa Azam, Lusajo Mwaikenda wakati wa mchezo wa Mzunguuko watatu wa Ligi Kuu uliopigwa mwanzoni mwa mwezi Septemba, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kiungo huyo aliyerejea Young Africans akitokea Simba SC, alitenda kosa hilo dhidi ya Lusajo Mwaikenda aliyekuwa ameanguka chini wakati wa harakati za kugombea mpira pembezoni mwa lango la Azam FC.

Kwa mantiki hiyo Morrison atakosa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting (Oktoba 3), Namungo FC (Oktoba 13) na Simba SC (Oktoba 23).

Wakati huo huo Kamati ya saa 72 imewapeleka Kamati ya Waamuzi ya TFF, Mwamuzi wa kati na msaidizi wake Franka Komba wa mchezo wa Mzunguuko watatu Young Africans dhidi ya Azam FC, na mchezo wa Mzunguuko wanne kati ya Tanzania Prisons vs Simba, Ahmed Arajiga, kwa ajili ya kujadiliwa baada ya kuonekana walishindwa kumudu michezo hiyo.

Mwamuzi msaidizi namba mbili wa mchezo wa Tanzania Prison Vs Simba Black Tubuke, naye amepelekwa kamati ya waamuzi ya kwa ajili ya kujadiliwa baada ya kuonekana kuwa alishindwa kumsaidia vema mwamuzi wa kati wa mchezo.

Kennedy Juma: Kocha Mgunda ananiamini
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 23, 2022