Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye, ambaye alizuiliwa kwa wiki kadha amepewa dhamana na Mahakama Kuu nchini humo.

Jaji Wilson Masalu Musene amempa dhamana  kiongozi huyo wa chama cha Forum for Democratic Change dhamana ya dola 30,000 za Marekani.

Hata hivyo amemtaka  Dkt Besigye kutojihusisha na vitendo vya kufanya ghasia na adumishe amani katika jamii hadi kesi hiyo ya uhaini inayomkabili isikilizwe na uamuzi kutolewa.

Dkt. Besigye ametakiwa awe anahudhuria mahakamani mara moja kila wiki mbili kuanzia Julai 26.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, wafuasi wa Beisgye wameimba wimbo wa taifa wa Uganda na kushangilia baada ya kiongozi wao kupewa dhamana.

Besigye amerejeshwa sero kusubiri kukamilishwa kwa utaratibu wa kumwachilia huru kwa dhamana hiyo.

Arsene Wenger Amtimua Thierry Henry Arsenal
Video: Rais Magufuli Azungumzia Taarifa Zilizosambaa kuhusu Mkurugenzi Aliyemteuwa