Mlinda mlango kutoka nchini Colombia David Ospina huenda akaihama klabu ya Arsenal, na kutimkia nchini Uturuki kujiunga na klabu ya Besiktas.

Ospina anapewa nafasi kubwa ya kuondoka kaskazini mwa jijini London, kufuatia hali ya ushindani iliyojengeka ndani ya kikosi cha Arsenal, baada ya kusajiliwa kwa mlinda mlango kutoka nchini Ujerumani Bernd Leno mwezi uliopita.

Ospina anaamini huenda akawa chaguo la tatu, kufuatia kusajiliwa kwa mjerumani huyo, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuwa chaguo la kwanza la meneja Unai Emery huku Petr Cech akitarajiwa kuwa chaguo la pili, endapo hatoondoka katika kipindi hiki.

Baada ya kukamilika kwa fainali za kombe la dunia, Ospina aliweka wazi hitaji lake la kutaka kuwa chaguo la kwanza, na tayari uongozi wa Besiktas umeonyesha nia ya kumtimizia lengo lake, kufuatia kuondoka kwa mlinda Fabri alietimkia Fulham ya England.

Mlinda mlango kutoka nchini Hispania na klabu ya Espanyol David Lopez alikua anapewa nafasi ya kusajiliwa na klabu ya Besiktas, lakini pendekezo lingine limeelekezwa kwa Ospina ambaye anaonekana kuwa na uwezo na mahiri mkubwa.

Ospina mwenye umri wa miaka 29, endapo ataondoka Emirates Stadium, atatoa nafasi kwa Petr Cech kusalia klabuni hapo, licha ya kuendelea kupewa nafasi ya kuuzwa katika kipindi hiki cha dirisha la usajili wa majira ya kiangazi.

Wanne mbaroni kughushi nyaraka 240 za serikali
Wafanyakazi wawili wa TTCL mbaroni kwa kuhujumu kampuni