Klabu ya Besiktas ya nchini Uturuki imoenyesha nia ya dhati ya kutaka kumsajili beki kutoka nchini Slovakia na klabu ya Liverpool, Martin Skrtel tofauti na ilivyo kwa Middlesbrough.

Besiktas, wamekua mstari wa mbele kuhakikisha wanaipata saini ya beki huyo ambaye thamani yake ya uhamisho ni Pauni milioni 7, kutokana na kuonyesha msisitizo kila kukicha wa kutaka kuanzwa kwa mazungumzo kati yao na majogoo wa jiji.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp, ameonyesha kuwa tayari kumuuza Skrtel, ikiwa ni sehemu ya kufanya maboresho ya kikosi chake kwa kuwasajili wachezaji wengine ambao anaamini wataendana na mfumo wake.

Hata hivyo pamoja na uongozi wa klabu hiyo ya nchini Uturuki kuonyesha dhamira hiyo, bado wanaweza kupata upinzani mkali kutoka kwa  Middlesbrough ambao wanachagizwa na hatua ya beki huyo mwenye umri wa miaka 31, kuhitaji kusalia nchini England.

Skrtel amedumu na klabu ya Liverpool kwa muda wa miaka minane baada ya kusajiliwa mwaka 2008 akitokea nchini Urusi alipokua akiitumikia klabu ya Zenit Saint Petersburg          .

Prof Tibaijuka: Aliyenipa fedha za Escrow hakuguswa
Elias Maguri Afikiria Kurudi Msimbazi