Mwanamziki staa wa pop na RnB Beyonce Knowles na mme wake rapa na mfanya biashara Sean Carter ‘Jay Z’ wamefanikiwa kupata watoto mapacha.

Japo wawili hao hawajaweka wazi jinsia za watoto wao mapacha na ni lini wamezaliwa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Beyonce amejifungua wiki moja iliyopita na alilazimika kubaki hospitali kwa muda akingoja utaratibu wa kitabibu.

Beyonce na Jay Z tayari wana mtoto wa kike anayeitwa Blue Ivy mwenye umri wa miaka 5 na wawili hao imekuwa furaha kwao kupata watoto mapacha.

Picha: Angalia Safari Ya Mwisho Ya Cheick Tiote
Ureno yatangaza siku tatu za maombolezo

Comments

comments