Mbunge mteule wa chama cha wananchi (CUF), Bi Hindu Mwenda amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu zaidi aliyokuwa akipatiwa.

Aidha, taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Abdul Kambaya imesema kuwa Bi Hindu amefariki jana jioni baada ya kuugua kwa siku kadhaa japo hajaeleza kiundani chanzo cha kifo chake lakini amesema taratibu nyingine zinazofuata zitaelezwa hapo baadaye.

Hata hivyo, Marehemu Bi Hindu alikuwa ni miongoni mwa wabunge wapya waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi ya wabunge nane ambao walivuliwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba

Video: Demokrasia Kenya ilivyoshangaza dunia
Jiwe kubwa tishio kwa Dunia, wanasayansi wahaha