Mama mzazi wa Diamond Platinumz ambaye ni Bi Sandra amesema siku ambayo mwanaye Abdul Naseeb maarufu kama Diamond Platinumz atapoamua kufunga ndoa na mama mtoto wake Hamisa Mobetto hatokanyaga katika harusi hiyo.

Bi sandra amesema kuwa Hamisa Mobetto hafai kuwa mwanamke wa kuwekwa ndani yaani ”Wife material” kutokana na mambo ambayo hayakumridhisha kipindi ambacho mlimbwende huyo aliishi nyumbani kwake Madale.

”Siwezi kukanyaga kwenye hiyo harusi hata siku moja watasherekea wenyewe” amesema Bi Sandra.

Hata hivyo Mama Diamond ameeleza kisa cha kutomkubali mama mtoto wa mjukuu wake Abdul ni kufuatia sakata la mwanadada huyo kuwaita Shilawadu kurekodi tukio lake la kumtembelea hospitali pindi alipojifungua mtoto wake, Abdul jambo ambalo lilipangwa kufanywa siri baina yao.

Aidha ameongelea swala la kuwarusha mtandaoni watoto wa Zarina Hassan Tiffah na Nillan zaidi ya ambavyo anampost Abdul ambaye ni mtoto wa Hamisa Mobetto, amesema kuwa bado anamuheshimu sana Zari kwani ndiye mwanamke wa kwanza kumfanya mwanaye Diamond Platinumz aitwe Baba.

”Ninamheshimu Zari kwa sababu ni mwanamke ambaye ndiyo wa kwanza kabisa kumfanya mwanangu aitwe baba” amesema Bi Sandra.

 

Video: DataVision International yaongeza tumaini la maisha kwa watoto
Video: Watoto 4000 majumbani kuanzishiwa tiba ya saratani

Comments

comments