Serikali ya Zimbabwe imesitisha shughuli za biashara nchini humo kufuatia ongezeko la maambukizi ya Covid-19, hatua inayowaweka katika hali ngumu raia wake wanaotegemea ajira ya sekta isiyo rasmi. 

Makamu wa Rais na Waziri wa afya Constantino Chiwenga amewaambia wanahabari kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa katika msimu huu wa sherehe ambalo liliongeza marudufu idadi ya maambukizi yaliyorekodiwa katika mwaka mzima. 

Amesema huduma muhimu kama vile hospitali, maduka ya dawa na maduka ya jumla ndio yatakayoendelea kutoa hudumakwa siku 30 zijazo, hali inayoongeza ugumu wa maisha kwa familia ambazo tayari zimekumbwa na umasikini.

Taifa hilo la kusini mwa Afrika tayari linakabiliwa na mgogoro mkali wa kiuchumi, mfumuko wa bei na kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira.

Agizo la Samia Suluhu kwa Uongozi wa mkoa Dodoma
Watu 56 wameuawa katika shambulizi la kigaidi- Niger