Mkutano wa mwaka wa G20 unaojumuisha mataifa yenye uchumi mkubwa duniani umemalizika nchini China, ukiongozwa na Rais Xi Jinping, amesema wajumbe wa nchi wanatakiwa kuimarisha nguvu mbili za kibiashara na uwekezaji.

Akiongea huko Hangzhou, Rais Xi amesema kutakuwa na makubaliano kupinga ulinzi wa soko. Amesema kuwa kwa mara ya kwanza mkutano huo umeweka masuala ya maendeleo mbele na kati.

Mkuu wa IMF, Christine Lagarde, amesema viwango vya ukuaji uchumi duniani umekuwa ukishuka kwa muda mrefu na wajumbe wa G-20 watatumia kila njia kuukuza.

Na tamko la mwisho limekubaliana na mataifa kuongeza usaidizi wa ubinadamu na na misaada kwa wakimbizi.

CUF walia na kauli ya JPM kuhusu mgomo wa Maalim Seif
Wabunge wa Upinzani Kuanza Vikao vya Kutafuta Suluhu na Naibu Spika