Takwimu za Biashara kati ya Nchi ya Tanzania na Nchi ya Burundi imeongezeka kutoka shilingi Bilioni 83.9 kwa mwaka 2015 hadi kufikia Bilioni 200.1 kwa mwaka 2019.

Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, wakati akizungumza na waandaishi wa habari nchini Burundi katika siku yake ya kwanza ya ziara ya siku mbili nchini humo, huku akielezea malengo ya ziara hiyo ni pamoja na suala la kukuza uhusiano wa kiuchumi hususani namna ya kukuza biashara na uwekezaji.

Aidha Tanzania imesajili miradi 18 kutoka Burundi yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 209.4 ambayo imetoa ajira 3544 kwa watanzania, moja ya mradi ni kiwanda cha mbolea chenye thamani ya shilingi milioni 180, huku Burundi pia ikiwa imesajili kampuni kutoka Tanzania kama vile Azam Ltd, Azania Ltd, na nyinginezo.

Hata hivyo Rais Samia amesema kuwa kiwango cha biashara na uwekezaji bado ni kidogo ukilinganisha na fursa zilizopo.

Sambamba na hayo Rais Samia maesema nchi zote zitaendelea kushirikiana kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa kuondoa vikwazo vya vya kodi na visivyo na kodi ikiwemo kuharakisha ujenzi wa kituo cha pamoja cha huduma za mpakani.

Infantino atuma salamu za pongezi Msimbazi
Kesi ya Sabaya mapya yaibuka