Uongozi wa Biashara United Mara umekanusha taarifa za kujihusisha na rushwa na kusababisha kikosi chao kushindwa kusafiri kuelekea Libya kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Kikosi cha Biashara United Mara kilishindwa kusafiri mwishoni mwa juma lililopita kuelekea mjini Tripoli, Libya kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili, ambao ulitarajiwa kuchezwa Jumamosi (Oktoba 23).

Uongozi wa klabu hiyo ya Mkoani Mara, umesikitishwa na taarifa hiyo na umeahidi kufanya uchunguzi wa kina ili kutambua chanzo chake, kisha kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria waliobuni uongo huo na kuusambaza kwa njia za mtandao.

Wakati huo huo Shirikisho la soka Barani Afrika ‘CAF’ halijatangaza maamuzi yoyote kuhusu sakata la kushindwa kusafiri kwa Biashara United Mara kuelekea mjini Tripoli, kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya wenyeji wao Al Ahly Tripoli.

‘CAF’ wanatarajiwa kutangaza maamuzi ya sakata hilo wakati wowote, ambayo yatatoa hatma ya Biashara United kwenye michuano ya Kimataifa, hasa ikizingatiwa Shirikisho la soka nchini TFF liliwasilisha ombi la mchezo wa mkondo wa pili uahirishwe kufuatia changamoto za safari zilizowakabili wawakilishi hao wa Tanzania.

Biashara United Mara ilichomoza na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam, Uwanja wa Benjamin Mkapa (ijumaa (Oktoba 15).

Watunza kumbukumbu wakumbushwa Usiri wa Nyaraka za umma.
Drake amiliki cha kuazima.