Mwenyekiti wa Klabu ya Biashara United Mara Suleyman Mataso, amekiri klabu hiyo kuwa katika hali ngumu ya kifedha, huku ikikabiliwa na changamoto ya safari ya kuelekea nchini Libya, kwa ajili ya mchezo wa Mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Tripoli.

Biashara United Mara itacheza mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Tripoli Oktoba 15, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mataso amesema wanaendelea kufanya mchakato wa kusaka fedha zitakazowawezesha kufanya safari ya kuelekea nchini Libya, kwa ajili ya mchezo wa Mkondo wa Pili utakaochezwa mwishoni mwa juma lijalo.

“Hali ni mbaya sana kwa ajili ya mchezo wetu wa marudio ugenini, kwa muda huu gharama za matumizi ya safari mambo hayajakaa sawa na hata tiketi pia bado hatujapata hivyo wadau watupe sapoti katika hili.” amesema Mataso

Kikosi cha Biashara United Mara tayari kipo jijini Dar es salaam, kwa ajili ya mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Tripoli, ambao wanatarajiwa kuwasili jijini humo wakati wowote kuanzia leo Jumatano (Oktoba 12).

Rais Samia aipa Maagizo PPRA, Fedha za IMF
Gomes awaita haraka Banda, Nyoni