Timu ya Biashara United ya mkoani mara iliyopanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao,  imeendelea kujiimarisha kwa kuingia makubaliano na kocha mpya Hitimana Thierry raia wa Rwanda.

Kocha huyo amejiunga na biashara united akitokea  timu ya Bugesera FC inayoshiriki ligi kuu nchini Rwanda.

Hitimana Thiery anakuwa kocha watatu raia wa Rwanda kusajiliwa kuifundisha timu ya ligi kuu Tanzania bara, baada ya Ally Bizimungu anayefundisha Mwadui pamoja na Kayiranga Baptiste wa Alliance Sports Club ya jijini mwanza iliyopanda daraja msimu huu.

Aidha, hivi karibuni Biashara United ilifanya usajili wa wachezaji wanne kutoka mataifa ya Guinea, Nigeria, Ivory Coast na Burkina Faso ikiwa ni sehemu ya kuimarisha kikosi chao.

Simba yamleta kocha mpya kimyakimya
Changamoto ya elimu yatajwa zao la Parachichi kukosa ubora Njombe

Comments

comments