Klabu ya Juventus Maarufu kwa jina la Bibi vizee imeweka historia katika ligi kuu nchini Italy kwa kutwaa ubingwa wa Ligi hiyo mara sita mfululizo huku ikiziacha timu nyingine midomo wazi.

Aidha, Juventus wametwaa ubingwa huo wa Seria A baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya vibonde wa ligi hiyo klabu ya Crotone ambapo mabao ya ushindi ya Juventus katika mchezo huo yalifungwa na mshambuliaji Mario Mandzukic katika dakika ya 12 ya mchezo , Paulo Dybala akaongeza bao la pili katika dakika ya 39, Mlinzi Alex Sandro akapiga msumari wa mwisho katika dakika ya 83.

Hata hivyo timu hiyo inajitwalia kombe la pili baada ya wiki iliyopita kutwaa taji la Copa italia kwa kuichapa Lazio kwa mabao 2 -0 hivyo kuonyesha mafanikio makubwa kwa msimu mzima uliomalizika.

Video: Mwigulu ateta na Polisi mauaji Kibiti, JPM atoboa siri bomba la mafuta
Real Madrid yatwaa ubingwa wa La Liga