Rais mpya wa Marekani Joe Biden ameanza kutengua sera kadhaa muhimu za Donald Trump, saa chache baada ya kuapishwa mbele ya jaji wa Mahakama Kuu John Robert.

Rais Biden alipishwa Januari 20, 2021, kuwa Rais wa 46 wa Marekani  na tayari amesaini maagizo ya watendaji 15 yanayolenga kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Amri nyingine ni kubadilisha msimamo wa utawala wa Trump juu ya mabadiliko ya hali ya hewa , uhamiaji na ukosefu wa usawa.

Shughuli ya uapisho wa kiongozi huyo na Makamu wake wa Rais, Kamala Harris, ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Barack Obama, Bill Clinton, George W Bush na aliyekuwa makamu wa Rais wa Trump, Mike Pence.

Emiliano Buendía kurithi mikoba ya Mesut Ozil
Haya hapa matarajio ya Chikwende Simba SC