Rais wa Marekani, Joe Biden anatarajia kukutana na mwenzake wa China, Xi Jinping, wiki ijayo nchini Indonesia kandoni mwa mkutano wa kilele wa kundii la mataifa 20 yenye uchumi unaokuwa, kwa mujibu wa Ikulu ya White House.

Mkutano huo, wa mjini Bali utakuwa wa kwanza kati ya viongozi hao wawili tangu Biden kutwaa urais Januari 2021. Unafanyika siku chache baada ya Xi kushinda muhula wa tatu, unaomuhakikishia kusalia madarakani kwa miaka mingine mitano ijayo.

Joe Biden na China, Xi Jinping. Picha ya AP.

Mahusiano baina ya Marekani na China yameathirika sana katika siku za karibuni. Ushindani wa kiteknolojia, uchokozi kwenye kisiwa cha Taiwan na uhusiano baina ya China na Urusi, ni miongoni mwa mambo yaliyochochea kuporomoka kwa ushirikiano baina ya pande hizo mbili.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema hatahudhuria mkutano huo wa G20 unaofanyika Novemba 15 na 16, 2022.

Sadio Mane atajwa safari ya QATAR
Marekani ya kwanza kuwasili QATAR