Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, wamefanya mazunguzo ya kutafuta maridhiano kufuatia mzozo juu ya makubaliano ya utengenezaji wa nyambizi.

Wakizungumza kwa njia ya simu ili kufikia makubaliano baina yao Marais wamefikia tamati ya kuendelea kuimairisha mashauriano kati ya serikali zao.

Hata hivyo hatua hiyo inapelekea kuweka mazingira ya kurejesha tena imani, na pia kutengeneza malengo ya pamoja.

Aidha Taarifa hiyo ya pamoja imesema kuwa Biden na Macron watakutana ana kwa ana barani Ulaya mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Balozi wa Ufaransa nchini Marekani pia anatarajiwa kurejea mjini Washington wiki ijayo, baada ya serikali mjini Paris kumrejesha nyumbani wiki iliyopita, kufuatia hasira juu ya kuanzishwa kwa ushirika wa ghafla kati ya Marekani, Uingereza na Australia, ambao ulihusisha Marekani kuisaidia Australia na nyambizi zinazotumia nguvu ya nyuklia.

Hata hivyo hatua iliyopelekea kufutwa kwa makubaliano ya euro bilioni 30 ambayo Australia ilikuwa imefikia na Ufaransa mwaka 2016 ya ujenzi wa nyambizi zinazotumia dizeli na umeme.

Milioni 700 kukarabati barabara ya Karagwe
Ramadhan Kayoko akabidhiwa fupa