Bidhaa zenye thamani ya shilingi milioni 200 zimekamatwa na Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) kwa kukosa kiwango cha uingizwaji nchini pamoja na kupitwa na muda.

Akitoa taarifa kwa wandishi wa habari mara baada ya ukaguzi wa  bidhaa hizo Mkaguzi Mkuu kutoka Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Suleiman Akida Ramadhani amesema bidhaa hizo zimekamatwa katika maeneo ya Shakani na Kwamchina.

Amesema, bidhaa hizo zimeingizwa kutokea nchini Ukrain na zimeingia Zanzibar bila ya kufanyiwa ukaguzi na Wakala husika jambo ambalo ni kinyume na utaratibu uliowekwa.

Aidah amesema kwamba bidhaa hizo hazikuwa na  vifungashio vyenye lugha inayofahamika ambapo amesema kuwa zimeshapitwa na muda na ni hatari kwa matumizi ya binadamu.

Akizitaja bidhaa hizo nipamoja na Tambi aina ya Pasta, makoronya, sabuni mbalimbali na biskuti ambazo zimeingia nchini mwaka 2019 na hazikuwahi kukaguliwa kupitia Wakala wa  Chakula, Dawa na Vipodozi.

“Mfanya biashara yoyote ni lazima akubali maagizo anayopewa na taasisi husika kabla ya kuingiza bidhaa nchini na sio kumuachia wakala kutoa mizigo kinyemela kwani hupelekea hasara pale zitakapoangamizwa” amesema Ramadhani.

Israel yatangaza tahadhari kuhusu Rais mpya wa Iran
Silinde: Natoa miezi miwili daraja lianze kujengwa