Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Ally Gugu amesema ziara ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini China, imepelekea bidhaa zaidi ya 8000 za Tanzania kuanza kuuzwa katika Taifa hilo bila ukomo na ushuru.

Gugu, ameyasema hayo katika Mkutano wa Wadau wa Viwanda na Uzinduzi wa Mfumo wa Taarifa za Biashara (Biashara App), uliofanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Ally Gugu.

Amesema, “Kutoka mwaka 2018 January tunapaswa kuuza bidhaa zetu bila ushuru wala kodi katika nchi 16 za SADC, tumepanua soko Afrika nzima ambapo tumelegeza masharti ya kibiashara.”

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Latifa Khamis alisema mfumo huo umezinduliwa ili kuisaidia jamii hasa wakulima kupata taarifa za bei za bidhaa.

Mwenyekiti CCM aongoza kikao Dodoma
Mkwasa afunguka kilichomtoa Ruvu Shooting