Muimbaji kutoka Canada, Justin Bieber amemvisha pete ya uchumba mwanamitindo Hailey Baldwin wikiendi iliyopita, chanzo cha kuaminika kimedhibitisha taarifa hizo.

Wawili hao ambao waliingia kwenye mahusiano mwaka 2016 wamefanya tukio hilo wakati wakiwa mapumziko kwenye visiwa vya Bahamas.

Bieber mwenye umri wa miaka 24 na Hailey, 21, wameonekana kufurahia mahusiano yao huku mashabiki wakishtushwa na taarifa hizo kama walivyo nukuliwa kupitia mitandao ya kijamii, wengi wakisema walitegemea Bieber anagemchumbia muimbaji Selena Gomes ambaye waliachana na kurudiana Octoba 2017.

Licha ya kuwa wawili hao hawajadhibitisha kuwa wameingia kwenye uchumba lakini baba mzazi wa Justin Bieber, Jeremy Bieber ni kama ameweka wazi juu ya taarifa hizo baada kuandika kwenye mtandao wa Instagram kuwa anajivunia ukurasa mpya aliouanza kijana wake.

‘’kujivunia ni kujishusha, nategemea makubwa kwenye ukurasa mpya’’ amendika baba wa mzazi wa  Justin Beiber  huku ujumbe huo ukisindikizwa na picha ya mwanae.

Hata hivyo, mwaka 2016 Bieber akifanya mahojiano na jarida la GQ alimzungimzia Hailey kwa kusema hataki kuwa na haraka kwenye mahusiano na mrembo huyo kwa kuwa huenda akawa ni mwanamke wake wa ndoa.

“Itakuaje kama kama Hailey ataishia kuwa msichana wangu ,nitamuoa sindivyo ? kama nikiharakisha kwenye kitu chochote, nitamuumiza, kisha yataendelea kuwa maaumivu, nivigumu kurekebisha vidonda vya namna hiyo, sihitaji kumuumiza “ alisema Bieber.

Lugola afunguka tena kuhusu watu wanaopotea
Young Killer afunguka mpango wa kuuza msemo ‘Pambana na Hali Yako’

Comments

comments