Mwimbaji mahiri wa kundi maarufu la muziki kutoka nchini Kenya, Sauti Sol Bien-Aime Baraza amejitosa rasmi katika ulimwengu wa biashara, ambapo kwa mara ya kwanza amethibitisha kufungua Klabu yake ya usiku na mgahawa unaoitwa ‘The Manhattan’.

Klabu hiyo mpya iko katika viunga vya jiji la Nairobi, kwenye moja ya majengo maarufu jijini humo la Imaara Mall lililozinduliwa hivi karibuni.

Mwishoni mwa juma lililopita, Bein akiwa na rafiki zake wachache walikuwa kwenye klabu hiyo kwa ajili ya uzinduzi rasmi, ambao uliambata na show yake ya kwanza akitumbuiza wimbo wake mpya ‘Inauma’ ambao umekuwa ukienea kwa kasi mitandaoni tangu kuachiwa kwake kwenye majukwaa mbali mbali ya kusikilizia muziki online.

Uzinduzi huo, uligubikwa na shangwe kubwa kutokana na kuhudhuriwa na watu mashuhuri nchini humo akiwamo mchekeshaji Eric Omondi, Makena Njeri, Eugene Mbugua, MC Antonio, Chiki Kuruka (mke wa Bien), Mchekeshaji Eddie Butita, Mchekeshaji Nick BigFish, Mcheshi Carlos Experience na wengine wengi.

Bein, pia alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwaarifu maelfu ya mashabiki wake kuhusu biashara hiyo, akiwaalika kujitokeza ili kumuunga mkono.

Mwanamuziki huyo nyota wa kundi la Sauti Sol, rasmi ameingia kwenye orodha ya watu wengine mashuhuri ambao wanamiliki vilabu vya usiku na migahawa katika ukanda wa Afrika Mashariki akiwamo nyota wa muziki kutoka Tanzania Rayvanny ambaye septemba 3, mnamo mwaka 2021 alifungua mgahawa wa kifahari.

Wolper atangaza kutarajia mtoto
Risasi yauwa wawili, 15 wajeruhiwa