Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Sam Allardyce ameandika waraka wa kuomba radhi baada ya kujizulu nafasi yake kufuatia kashfa ya mbaya inayomkabili.

Allardyce ambaye amedumu katika kazi ya ukocha wa timu ya taifa kwa muda wa siku 67 tu tangu abebe majukumu hayo, nafasi yake imezibwa kwa muda na meneja wa kikosi cha Uingereza chini ya miaka 21 Gareth Southgate na kumalizia michezo yote iliyosalia.

“Ilikuwa ni heshima kubwa kwangu kuteuliwa kuwa kocha wa wa kikosi cha Uingereza mwezi July na kwa hakika nimesikitishwa sana na jambo hili.

“Jioni ya leo (jana), nimekutana na Greg Clarke na Martin Glenn na kueleza azma yangu ya kuomba msamaha kwa tukio lililotokea.”

“Japokuwa nimeweka wazi kwenye yale mazungumzo yaliyorekodiwa kwamba maafikiano yale yangehitaji uthibitisho ama kupitishwa na FA, lakini natambua nimetoa baadhi ya kauli ambazo zimeumiza watu,” Allardyce amezidi kuelezea.

“Nikiwa kama moja ya watu waliohudhuria kikao cha leo (jana), niliambiwa nitoe ufafanuzi juu ya nilichokieleza na eneo ambalo mazungumzo hayo yalifanyika. Na nimetoa ushirikiano mkubwa sana kwenye suala hilo.

“Vilevile najutia sana kauli zangu hasa kwa kumlenga mtu mmoja-mmoja.”

Timu ya taifa ya Uingereza itavaana na Malta kwenye mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia Oktoba 8, tayari wakiwa wameshinda mchezo mmoja dhidi ya Slovakia kwa bao 1-0 wakati huo Allardyce akiwa kwenye bechi la ufundi.

Katibu Tawala, Muhasibu Mkuu na Mkurugenzi wa halmashauri ya Bukoba ni majipu
Kampuni tisa za Korea Kusini kuwekeza Tanzania