Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imeidhinisha Tsh. Bilioni 20 za madeni ya wakulima wa korosho, wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ikiwa ni baada ya wataalamu kuhakiki madeni ya zaidi ya Tsh. Bilioni 23.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wa AMCOS huko Matogoro, Tandahimba Mkoani Mtwara alipoenda kuhamasisha maandalizi ya msimu wa ununuzi wa korosho.

“Rais Magufuli alitoa fedha hizi kwaajili ya Tandahimba, Masasi, Mtwara na Kibiti kwaajili ya waliokuwa wamelipwa nusu, waliolipwa kiasi, na wasiolipwa kabisa, fedha hizi zitaanza kulipwa kesho asubuhi” amesema Wazri Mkuu.

Amesema fedha hizo zimetokana na mfumo uliotengenezwa na wanunuzi ili kumnyonya mkulima katika msimu wa 2018/2019 kwa kununua kilo ya korosho kwa Tsh. 1,500 badala ya Tsh. 3,000 hali iliyolazimu Serikali kuingilia kati na kuamua kuzinunua korosho zote.

Katika hatua nyingine amevitaka vyama vikuu vya Ushirika na AMCOS kuweka kipaombele cha kununa mashine ndogo ndogo za kubangulia korosho ili waache mtindo wa kuuza korosho ghafi.

Kuhusu msimu wa ununuzi wa koshosho mwaka huu, Waziri Mkuu amesema unaanza Septemba hadi Desemba na akawataka viongozi wa ushirika wasimamie ununuzi wa korosho mapema.

Mchujo wagombea Ubunge CCM kuanza leo
Siku ya tatu mjadala kufufua uchumi EU