Mgombea urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi (CCM),  na rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameahidi kujenga uwanja wa ndege mkoani Mara iwapo atafanikiwa kuongoza kwa muhula wa pili.

Magufuli ametoa ahadi hiyo wakati alipomkaribisha mjane wa baba wa Taifa mama Maria Nyerere katika  kampeni za chama hicho mkoani Mara kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu.

 “Mzee Nyerere amezaliwa hapa, akatuleta pamoja Watu wa Dini na rangi zote ni lazima tumuenzi, katika utawala wangu Mungu akijalia yote aliyopanga Baba wa Taifa kuyatimiza, nitayatimiza kwa speed kubwa na pia kuendelea kuuenzi mkoa huu aliotoka” amesema Magufuli.

“Nimetangaza tenda kumpata mkandarasi, pesa zipo zaidi ya Tsh. Bil 49 kwa ajili ya kujenga uwanja wa ndege hapa tena wa lami, ili ndege ziwe zinatua, haiwezekani mama Maria Nyerere akitaka kwenda DSM awe anasafirishwa hadi Mwanza kupanda Ndege ” ameongeza Magufuli.

“Tumekamilisha hospitali ya kumbukumbu ya Mwl.nyerere, imeanza kazi Aug 31, nimeambiwa mpaka sasa wamezaliwa watoto 31 na mmoja anaitwa Julius kwa heshima ya Nyerere,tulitoa zaidi ya Tsh.Bil 15, hivi karibuni hospitali hii itaanza kusafisha figo” amesema Magufuli akiwa katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkoani Mara, leo Septemba 5, 2020.

Magufuli anatarajiwa kuwepo mkoani Mwanza kuendelea na kampeni kesho jumapili Septemba 6.

wakulima kulipwa mabilioni
Rungwe :Nitaendesha serikali yenye haki kwa kila mtu