Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Suleiman Jaffo amesema kuwa bila kusimamiwa kwa maadili katika jamii taifa litashindwa kusonga mbele katika juhudi za kujenga jamii inayochukia rushwa.

Ameyasema hayo wakati akizindua Maadhimisho ya Maadili ya Kitaifa Mjini Dodoma ambapo amewakemea viongozi wote wanaokumbatia rushwa na kuziagiza mamlaka zinazosimamia maadili kuwachukulia hatua kali ili kupunguza tatizo hilo nchini.

Kwa upande Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG, Prof. Mussa Assad amesema kuwa taasisi hiyo inaendelea kusimamia maadili na kupambana na rushwa pamoja na kusimamia maadili na haki za binadamu, hivyo kuendelea kuboresha ufanisi kwa jitihada za serikali.

Hata hivyo, kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni wajibika piga vita rushwa zingatia maadili haki za binadamu na utawala bora kuelekea uchumi wa kati.

 

Video: Mama Samia alivyotinga hospitali kumuona Lissu, Moto zaidi wawaka rushwa boss Takukuru
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 29, 2017